Deuteronomy 16:18-20

18 aWateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambao Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa. 19 bMsipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki. 20 cMfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa.

Kuabudu Miungu Mingine

Copyright information for SwhKC